Chama Cha Wafanyakazi
Tunapigania haki za wafanyakazi wa nyumbani Tanzania. Akina dada wa nyumbani, madereva, walinzi, wapishi, na wahudumu, n.k
Tunapigania haki za wafanyakazi wa nyumbani Tanzania. Akina dada wa nyumbani, madereva, walinzi, wapishi, na wahudumu, n.k
Asanteni sana kwa maoni wapendwa. Utamu wa demokrasia ni kwamba kila mtu ana sauti. Na maoni na mawazo ya wananchi ndiyo yanayowezesha uundaji wa sera bora. Pasipokuwa na kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa nyumbani, ndugu zetu watazidi kunyanyaswa; na uchumi wa Tanzania utazidi kududumaa, kwa sababu hakutokepo na middle class ya kutosha inayohitajika kukuza matumizi ya ndani ya nchi. Wafanyakazi wa nyumbani ni asilimia kubwa sana ya soko la ajira Tanzania- bila kuwanyanyua wao uchumi wa Tanzania hauwezi kukua, taifa letu litabaki kuwa maskini.
Naamini kuwa asilimia kubwa ya soko la ajira Tanzania ni wafanyakazi wa nyumbani, walinzi, madereva, na wapishi na wahudumu mahoteli.
Hii inamaanishi kuwa wafanyakazi tukiamua kujikusanya na kujipanga katika mfumo huu wa demokrasia- basi kweli kwa idadi yetu hii nguvu na mamlaka tunayo ya kupitisha sera bungeni kupitia wizara ya kazi na ajira, sera zitakazo weza linda haki na masilahi yetu.
Sera kama kima cha chini, masaa ya kazi, masaa na malipo ya sikukuu na wiki endi, pamoja na bima ya afya. Haya ndiyo ya muhimu kwa sasa.
Mfanyakazi inapaswa aweze tengeneza hela ya kutosha katika maisha yake ya kazi, ili ukijafika muda wa kustaafu- msingi wake wa kiuchumi tayari upo.
Tunapigania haki za wafanyakazi wa nyumbani Tanzania. Akina dada wa nyumbani, madereva, walinzi, wapishi, na wahudumu wa hoteli.
Tunaamini kuwa kutokana na mfumo wa uchumi wa kisasa kima cha chini cha mfanyakazi wa nyumbani Tanzania inapaswa kuwa Tsh. 500,000. Na pia mhajiri apaswa amuheshimu mhajiriwa na amntendehe haki zake za kibinadamu.
Tuungane pamoja ili tuweze simamia haki za wafanyakazi wa nyumbani Tanzania. Mualike mwenzako ili tuweze simama pamoja katika jitihada hii- umoja ni nguvu.
Kama mhajiri wako amekunyima haki zako za kibinadamu leo hii, basi wasiliana nasi ili sheria iweze chukuliwa.
Tunataka sera zipitishwe bungeni kwa kupitia wizara ya ajira na kazi- sera zitakazoweza walinda wafanyakazi wa wanyumbani- ambao kutokana na hali yao yaki jamii na uchumi unakuta wapo katika hatari ya kunyanyaswa, kuteswa, na kunyimwa haki kazini- pasipokuwa na sera za ajira zinazowalinda.
Sera kuhusu kima cha chini, pamoja na masaa ya kazi, pamoja na malipo na masaa ya wiki endi na sikukuu, pamoja na bima ya afya.
Pasipokuwa na sera za kuwalinda wafanyakazi wa nyumbani watanyanyaswa, na mwisho wa siku kunakuwa hakuna tofauti kati ya mtumwa na mfanyakazi.
Mfanyakazi siyo lazima umuweke alale nyumbani kwako. Unaweza kumuajiri na kumlipa kwa saa au kwa siku. Laki tano kwa mwezi kwa mahesabu ya siku itakuwa maeneo ya Tsh. 17,000. Bila kuwanyanyua wafanyakazi Tanzania uchumi utashindwa kukua, kwasababu asilimia kubwa ya soko la ndani pesa za matumizi ya kawaida wanakosa.
Kazi ya mfanyakazi wa nyumbani inaumuhimu na heshima sawa tu na kazi ya mwajiri- bila mfanyakazi wa nyumbani kufanya kazi yake mwajiri atashindwa kwenda kazini na kuingiza kipato.
We use cookies to analyze website traffic and optimize your website experience. By accepting our use of cookies, your data will be aggregated with all other user data.